Vipengele vya Mradi

Sehemu 1: Kuongeza usalama wa milki za Ardhi. Sehemu hii itasaidia utoaji wa hati milki za kimila, hati milki, leseni za makazi na shughuli zingine zinazohusiana. Shughuli katika kipengele hiki zitafanyika katika njia ya umoja na shirikishi ili kuhakikisha usawa wa kijinsia, na ulinzi wa haki za makundi yote ikiwa ni pamoja na wanawake, vijana, wawindaji na wakusanyaji, wafugaji, wakulima, nk. Mikoa mbalimbali na Halamshauri za Wilaya zitahusika katika utekelezaji wa mradi huu ikiwa ni pamoja na: Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Tabora, Geita, Pwani, Mwanza, Shinyanga, Tanga na Morogoro. Halmashauri za Wilaya ni pamoja na Dodoma (Chamwino), Simiyu (Maswa), Ruvuma (Mbinga), Katavi (Mpanda), Songwe (Songwe) na Momba Vijijini. Sehemu hii itajumusisha kufanyika kwa shughuli mbalimbali ambazo ni zimeelezwa hapa: -

Sehemu ndogo ya 1.1: Kutoa kwa wingi hati milki za kimila za ardhi katika maeneo ya Vijiji. Sehemu hii italenga kuongeza ufanisi katika maeneo ya majaribio ambayo itasaidia katika utekelezaji wa moja kwa moja katika utoaji wa hati milki za kimila. Hii inahitaji, ufafanuzi wa awali wa mipaka ya Vijiji, mipango ya matumizi bora ya ardhi, ushiriki wa wananchi katika upimaji wa mipaka ya vijiji pamoja na utatuzi wa migogoro na utoaji wav yeti vya Vijiji.

Sehemu ndogo ya 1.2: Kutoa kwa wingi hati milki na leseni za makazi katika maeneo ya Mijini. Sehemu hii ya utoaji wa hati milki mijini itahusisha michakato miwili tofauti yenye matokeo tofauti: mchakato wa urasimishaji utakaozalisha leseni za makazi 1,000,000 na mchakato wa upangaji na upimaji utakaozalisha hati milki 1,000,000. Urasimishaji wa ardhi kwa njia ya utoaji wa leseni za makazi utahusisha makubaliano ya maslahi katika kipande cha ardhi husika, kuandaa masijala ya ardhi ya mijini na utoaji wa leseni za makazi. Vile vile, mchakato wa upangaji na upimaji wa makazi holela na utoaji wa hati milki, utahusisha uzalishaji wa mipango ya urekebishaji makazi ili kuhakikisha inafuata viwango vya chini vya upimaji mijini (upana wa mitaa na njia, upatikanaji wa nafasi za umma kama vile shule na huduma nyingine).

Sehemu ya 2: Kuboresha mfumo wa usimamizi wa taarifa za ardhi nchini. Kipengele hiki kitajumuisha uboreshaji na usambazaji wa mfumo unganishi wa taarifa za ardhi (ILMIS) katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini, maboresho ya mtandao wa jiodesia, upigaji wa picha za anga, uchoraji wa ramani za msingi, na kuanzishwa kwa miundombinu ya utunzaji wa kumbukumbu za kijiografia (NSDI) ili kuimarisha upatikanaji na ufanisi wa huduma za utawala wa ardhi. ILMIS imefanyiwa majaribio na mradi huu utaiboresha na kuiimarisha zaidi, kusambaza mfumo huu katika maeneo ya mradi kwa njia bora ili kufikia sehemu zote za Nchi kwa ajili ya kuboresha taarifa za ardhi. Mfumo ulioboreshwa wa Jiodesia na ramani za msingi utasaidia sio tu shughuli za usajili wa ardhi lakini pia upatikanaji wa ramani za maeneo ambazo zitasaidia katika shughuli za kijamii, kiuchumi na kimazingira. Kipengele hiki kinajumuisha vipengele vidogo vifuatavyo: -

Sehemu ndogo ya 2.1: Kuboresha na kuusambaza mfumo wa ILMIS katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Sehemu hii itagharamia awamu ya pili uuandwaji wa mfumo ILMIS kwa kuboresha usimamizi wa pamoja wa hati milki za kimila, hati milki, na leseni za makazi, ikiwa ni pamoja na usajili wa awali na shughuli zilizofuatia. Usambazaji wa mfumo wa ILMIS utatekelezwa katika Mikoa 26 ambapo majengo ya ofisi yatajengwa na kuwekewa miundo mbinu itayosaidia utumiaji mfumo wa ILMIS.

Sehemu ndogo ya 2.2: Uzalishaji wa ramani za msingi. Kipengele hiki kitagharamia uzalishaji wa ramani za msingi kwa kutumia picha anga zenye ubora wa hali ya juu za hivi karibuni au picha za angani katika maeneo ya mradi na Wilaya ambazo ziko karibu na Wilaya lengwa za mradi ili kusaidia utoaji wa hati milki kwa wingi nchini, mipango ya matumizi bora ya ardhi pamoja na usimamizi wa ardhi.

Sehemu ndogo ya 2.3: Kuimarisha mfumo wa Jiodesia. Kipengele hiki kitasaidia kuanzishwa kwa vituo vya upimaji masaa yote (CORS) pamoja na miundombinu yake na alama za msingi za upimaji zenye ubora zitakazo saidia katika shughuli za upimaji kwa kutumia mtandao wa upimaji unaotumia satelaiti Duniani wenye gharama nafuu katika matumizi na matengenezo.

Sehemu ya ndogo 2.4: Maboresho ya Mifumo ya Uthamini: Sehemu hii itahusisha kuandaa ramani ya viwango vya thamani ya ardhi nchini, kuandaa kanzi data ya taarifa za uthamini ambazo zitatumika katika uthamini kwa ajili ya fidia, kodi nk.

Sehemu ya 3: Kuimarisha uwezo wa Wizara na taasisi zake: Sehemu hii itajumuisha maboresho ya sera, sheria na kanuni za ardhi, kuwajengea uwezo watumishi wa sekta ya ardhi, kuelemisha umma kuhusiana na masuala ya ardhi ili kuboresha utoaji wa huduma za utawala wa ardhi ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa na ujenzi wa ofisi ili kusambaza mfumo wa ILMIS, na kuimarisha Mabara ya Ardhi na Nyumba. Kipengele hiki kinajumuisha vipengele vidogo vifuatavyo:-

Sehemu Ndogo ya 3.1: Maboresho ya sera, sheria na kanuni. Kipengele hiki kitasaidia kuhuisha na kuunganisha Sera, Sheria na Kanuni kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika utawala wa ardhi na usajili. Hii itafanyika kupitia uchambuzi, warsha na ushauri kama itahitajika.

Sehemu Ndogo ya 3.2: Kujenga uwezo kwa watumishi wa sekta ya ardhi. Kipengele hiki kinalenga katika kuwajengea uwezo wadau wote muhimu katika ngazi ya Makao makuu na Halmashauri. Hii itahusisha mafunzo kwa wafanyakazi katika nyanja mbali mbali za maendeleo ya sekta ya ardhi na walio ndani ya mradi. Itafanyika tathmini ili kuona kama kutakuwa na uhitaji wa mafunzo.

Sehemu Ndogo ya 3.3: Kuimarisha Mabaraza ya Ardhi na Nyumba: kipengele hiki kitasaidia uanzishwaji na uendeshaji wa Mabaraza ya Kata ili kuongeza Mabaraza mapya, kuongeza rasilimali watu na fedha kwa mabaraza yaliyopo, kupunguza kesi, kuandaa miongozo katika ngazi ya Vijiji, Kata pamoja kutoa mafunzo na Vifaa.

Sehemu Ndogo ya 3.4: Maendeleo yanayoonekana ya Utawala wa Ardhi: Kipengele hiki kitasaidia katika ujenzi wa majengo ya ofisi katika Mikoa 26 na ukarabati wa Ofisi za Wilaya 12 zitakazotumika kwa ajili ya mfumo wa ILMIS. Pia litajengwa jengo la Kitaifa la kumbukumbu za ardhi. Kipengele hiki pia kitahusika na manunuzi ya vifaa muhimu kwa ajili ya majengo haya na kuhakikisha vifaa kwa ajili ya mtandao vinafungwa katika ofisi hizo. Aidha, mkakati wa utunzaji kumbukumbu utaandaaliwa.

Sehemu Ndogo ya 3.5: Uhamasishaji wa umma ili kujenga uelewa wa mradi: kipengele hiki kinalenga kujenga uelewa mpana wa utawala wa ardhi, shughuli za mradi wa LTIP, Sera zinazohusiana na ardhi, matakwa ya kisheria, na mifumo ya taarifa za ardhi kwa wadau mbali mbali. Maeneo mengine ya utekelezaji itajumuisha maandalizi ya mifumo ya mawasiliano, ufikishaji wa taarifa na kupima uwezo juu ya uelewa wa mifumo ya utawala wa ardhi. Shughuli zingine ni pamoja na mafunzo kuhusu utunzaji wa hati za ulinzi wa usalama (yaani ESMF, VGPF, SEP na RPF) kwa wadau mbalimbali katika ngazi tofauti katika kipindi cha utekelezaji wa mradi.

Sehemu ya 4: Usimamizi wa Mradi: katika muktadha huu, kitengo cha uratibu wa mradi (PCU) kimeanzishwa ndani ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kazi muhimu zitakazotekelezwa na PCU ni uratibu wa mradi, manunuzi, usimamizi wa fedha, usimamizi wa mazingira na masuala ya kijamii, pamoja na ufuatiliaji na tathmini. Ni muhimu kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara kwani mradi huu ndio mradi wa kwanza unaojitegemea unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na kutekelezwa na Wizara. Uwezo uliopo ndani ya Wizara utaimarishwa ili kuhakikisha utekelezaji wa mradi wenye mafanikio. Aidha, vifaa, ajira na mafunzo vitatolewa na kuboreshwa ili kuongeza uwezo wa Wizara.

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo