WENYEVITI WA MITAA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA MABILIONI YA URASIMISHAJI
Imewekwa: 23 May, 2024
WENYEVITI WA MITAA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA MABILIONI YA URASIMISHAJI

Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ya Dar es salaam wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha Shilingi Bilioni 345 kwa ajili ya kuongeza usalama wa milki za ardhi kwa kupanga, kupima na kumilikisha wananchi ardhi mijini na vijijini, kuboresha mifumo ya usimamizi wa taarifa za ardhi nchini na kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji.

 

Wenyeviti hao wamewataka wananchi wa jijini Dar es salaam kuwa tayari kwa kazi inayoendelea ya ukwamuaji wa Urasimishaji wa makazi ambayo hayaja rasimishwa hadi sasa na makampuni mbalimbali ya urasimisha yaliyokwama kukamilisha kazi hizo na kushindwa kuwapa wananchi hati zao za kumiliki ardhi.

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo